Wednesday, August 18, 2010

Shein: Sitaogopa, mimi si legelege

MGOMBEA wa urais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein amesema, akishinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ataiongoza Zanzibar bila ya woga, chuki wala jazba na amesisitiza kwamba ukimya wake haumaanishi kuwa ni legelege.

Dk. Shein ameahidi kumheshimu kila Mzanzibari iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Serikali ya Zanzibar (SMZ).

Mwanasiasa huyo ni Makamu wa Rais wa Tanzania,ametangaza msimamo huo leo wakati anazungumza na wagombea wa nafasi za ubunge, uwakilishi, udiwani na ubunge wa Viti Maalumu mjini Zanzibar.

Amesema, anaamini kuwa hizo ni sifa za kiongozi na kusisitiza kwamba hatakuwa pamoja na
mtu au kiongozi anayetumikia serikali kwa maslahi yake binafsi.

“Nikishinda, katika serikali nitakayoiongoza sitakuwa pamoja na mtu anayeitumikia
serikali kwa maslahi yake binafsi.Zanzibar tutaiongoza kwa misingi ya utawala bora
kwani ni nchi ya matumaini ya Wazanzibari wote,” alisema Dk.Shein katika mkutano huo.

Dk.Shein leo anatarajia kuchukua fomu ya uteuzi rasmi kutoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

No comments:

Post a Comment