Na Heri Shaaban,jijini
MANISPAA ya Ilala imeanza kampeni endelevu ya kupima mambukizo ya virusi vya UKIMWI (HBCT) kwa kila kaya zilizopo ndani ya manispaa hiyo.
Hayo yalisemwa jana na Mratibu wa Huduma za Afya na Jamii wa manispaa hiyo, Sofia Mtomola wakati wa akizungumza na gazeti hili kuelezea mafanikio ya manispaa hiyo kwa kipindi cha mwaka 2009 hadi Juni 2010.
Matomola amesema kuwa kampeni hiyo imeweza kuwafikia wakazi 9169 kutoka kata sita za manispaa hiyo na ambapo waliokubali kupima wakazi 9009.
Amesema kuwa kati ya wakazi hao waliokubali kupima afya zao majumbani mwao ni wanaume 4518 na wanawake 4657.
''Mpango wa kupima mambukizo ya UKIMWI ujulikanao kama Home Based Counselling and Testing ni endelevu na malengo ya mansipaa ni kupima katika kata zote 24 zilizopo Ilala, ''alisema Matomola.
Aodha ofisa huyo amewataka wakazi wa manispaa hiyo kutoa ushirikiano kwa kila mmoja ili kuwezesha kampeni hiyo ya upimaji wa kaya kwa kaya.
Ameongeza kuwa Serikali Kuu imebuni mbinu hiyo ya kutoa huduma majumbani, kufuatia idadi ya wananchi kujitokeza wachache katika vituo vya upimaji.
Soma Dar Leo
No comments:
Post a Comment