Tanzania ni miongoni mwa nchi zitakazokuwa za kwanza kunufaika na ugunduzi mpya wa chembechembe zenye uwezo wa kudhibiti virusi vya ugonjwa wa UKIMWI Kutokana na kutoa mchango mkubwa katika utafiti huo.
Mkurugenzi wa mpango wa utafiti wa dawa na tiba katika taasisi ya nchini marekani inayoshughulikia magonjwa ya kuambukiza na athari zake (NIAID), Dk.Margaret Johnstone amesema kuwa,Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zitanufaika mpema baada ya kukamilika kwa mchakato huo wa kupatikana dawa hiyo kutokana na kuwa na ushiriki kamili katika utafiti wake.
kutoka gazeti: Mwananchi
No comments:
Post a Comment