Tuesday, September 20, 2011

CHAGUZI ZA SIASA

hii ni changamoto kwa Watanzania kwenye siasa. Tunajua ushabiki ni moja ya tabia za binadamu, na kuwa kwenye chama na mtazamo tofauti ni haki yake. kwa kutambua hayo ndio maana kuna taratibu zinazowekwa kufuatwa ili kuepusha migogoro.

kinachosikitisha ni kuvunjwa kwa taratibu hizo. Tamaa na ubinafsi na uroho wa madaraka ndio tatizo.

Ni dhahiri wanosababisha vurugu ni viongozi wetu wanaotaka kupindisha sheria au haki za wananchi.

wanatumia udini,ukabila kuwagawa watu nakusababisha mvurugano.
Unafiki wa wanotumika na wanasiasa ni mbaya sana , kwa kweli utatumaliza na kutufanya tufarakane kwa sababu ya watu wa chache wajanja.

hongo ya elfu kumi, laki haiwezi lipa Amani na upendo uliojengwa mioyoni mwa Watanzania.

nachelea kusema kuwa tunaonekana wajinga kwa walio endelea, tunaidhalilisha nchi na viongozi wake.
kama kiongozi usijisikie fahari wakati wananchi unaowaongoza wapo katika hali mbaya kiakili, kimwili na kiroho.

Watanzania Tuamke!!

No comments:

Post a Comment